P-Square walitawala vichwa vya habari kwenye redio, TV, magazeti na blogs za Afrika kwa kuingia kwenye vita vikubwa vya maneno kati yao kiasi cha kundi kudaiwa kuvunjika.
Peter hadi alianza kufanya show zake mwenyewe kwa jina la Mr P ikiwa ni pamoja na kuanzisha management yake baada ya kukataa kufanya kazi na kaka yake Jude Okoye. Paul naye tayari ana label yake mwenyewe, Rudeboy Records.
Na sasa huenda mambo yamerudi kawaida. Mapacha hao wapo Afrika Kusini walikoenda kushoot video ya wimbo walioshirikishwa na Diamond Platnumz. Wote kwa pamoja wamepost picha Instagram japo Diamond bado hajapost chochote.
Mwanzoni wengi walidhani ni video yao wenyewe kabla ya Paul kupost picha mpya asubuhi ya leo akiwa amevaa kofia ya WCB na kuandika: t was great supporting a brother from east Africa ….. The king of east Africa, guess you already know who?”
“Dunno what we doing but we definatly having fun in jo’burg,” Paul aliandika kwenye ya picha aliyopost awali.
Naye Peter aliandika: We run thinz… Thinz don’t run we!! #killingIt #AllBlack #koolestDudes.
Hawa jamaa walikosana kweli au walitupiga changa la macho? You never know.. Wanasema usiamini kila kitu unachoona kwenye internet.
Mtangazaji wa Times FM, Lil Ommy ameandika mtazamo wake pia baada ya kuona picha hizo.
“Nafurahi kuona wapacha wa kundi kubwa la Muziki Africa kufanya kazi tena pamoja, wapo Johannesburg, South Africa wakifanya video Mpya,” ameandika.
“Sasa sijajua ni ngoma yao au yule mtoto wa Tandale ndo anafanya nao? Kama ni chibu amewakusanya hawa jamaa atakuwa katisha sana sababu hivi karibuni tuliona jamaa walikuwa na tofauti Peter alikuwa anafanya show kivyake na Paul alikuwa busy na Muno na Lucy #RudeBoyRecords it seems jamaa wameweka mambo yao sawa baada ya kuona picha hii instagram kwenye account zao ambayo inaonesha janaa wako on set.”
“Nilifanya interview wiki 2 zilizopita na Mkongwe wa Muziki Nigeria 2baba (2Baba) @official2baba na nilipomuuliza anachukuliaje kuona PSquare hawafanyi kazi pamoja tena kama zamani? Na Je alifanya chochote kusema nao hivi? 2Baba alisema ‘Hatujapendezwa na ishu hiyo, mimi sina upande wowote, kila mtu ana upande wake wa stori, wote ni washkaji zangu nimeongea nao tu kishkaji lakini wao wenyewe wanaokana wana nia ya kumaliza tatizo’ Sasa sijui kama ilikua ni kiki wanatengeneza au walizinguana mazima! Kama ni kiki basi wamefeli wangesubiri goma lipo tayari wanalibutua tu kuliko saivi picha zimeshavuja ikija tukutoa kiki imeisha isha,” ameongeza.
“Ile ule msala wao wa safari hii ulikua mziki! Sijui kama ni kiki. Peter alikaza! Katika kuonesha kuwa kama jamaa wako peace saivi, Peter ambae ndo mtata zaidi hivi amepost picha ya kaka yao Jude Okoye kumtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa ambayo ni leo pia. Kwa jinsi picha zinavoonekana kama vile bro wao hayupo nao SA kitu ambacho sio cha kawaida! coz yeye ndo huwa director wa video zao karibuni zote, may be madogo wameanza kwanza kuyamaliza wao then wamvute bro wao! Who knows? Time will tell.”
“Jude haja post chochote mpaka ss kuhusu kufanyika kwa video hii kwenye page yake. Wala Diamond @diamondplatnumz hajaweka picha yoyote akiwa nao on set kwenye page yake.Ingawa kuna collabo yake inakuja pia. So kama ni wao wamerudi pamoja well and good, S/O to @rudeboypsquare & @peterpsquare ila kama ni yule mtoto Dangote kawasogeza bondeni yani yeye ndo amewakutanisha kwa ajili ya video yake basi anatakiwa kupata heshima kubwa na headline itabadilika utasikia magazeti ‘Diamond awapatanisha PSquare.”
Post a Comment