Wiki tatu kabla ya kifo cha Papa Wemba, Jumapili ya jana, Diamond alirekodi wimbo naye jijini Paris, Ufaransa.
Akiwa kwenye ziara yake ya Ulaya, Diamond alienda Paris na kuingia studio na msanii huyo kurekodi wimbo huo alioshirikishwa. Hakusema awali kwakuwa kilichobainika kwenye safari hiyo ni kuingia studio na Fally Ipupa aliyemshirikisha.
Diamond amepost video inayowaonesha wawili hao wakiwa studio baada ya kurekodi wimbo. Wimbo huo unasikika kwenye video hiyo chini.
“Wiki nne tu zilizopita tulikuwa Paris, akanishirikisha kwenye nyimbo yake, tukapanga mengi juu ya wimbo halaf ghafla naskia habari ya Msiba…Dah! nimesikitika sana, Hakika binadamu ni wazungumzaji tu ila Mwenyez Mungu ndio Mpangaji…Pumzika salama Kiongozi wetu daima tutakukumbuka, #RipPapaWemba,” ameandika Diamond.
Papa Wemba alifariki Jumapili hii baada ya kuanguka jukwaani alipokuwa akitumbuiza kwenye tamasha kubwa nchini Ivory Coast.
Post a Comment